Yemen yalaani ugaidi wa kiserikali wa utawala wa Israel

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Yemen amelaani ugaidi wa kiserikali unavyofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya taifa lisilo na ulinzi la Palestina.

Mji wa Nablus unaendelea kuzingirwa na jeshi la utawala haramu wa Israel kwa siku ya 15 mfululizo, na zaidi ya hayo, idadi kubwa ya raia wamekamatwa katika maeneo tofauti ya Ukingo wa Magharibi na Baitul Muqaddas.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Yemen, Hisham Sharaf Abdullah, sambamba na kulaani ugaidi wa kiserikali unaofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina, ametahadharisha kuhusu kushadidi mivutano baina ya pande hizo mbili.

Ametaja hujuma zinazofanywa na askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina kuwa ni tishio la moja kwa moja kwa amani na usalama wa kimataifa na amelitaka Baraza la Usalama kuchukua jukumu la kuwalinda Wapalestina wanaokabiliwa na mashambulizi mabaya zaidi ya Wazayuni.

Katika siku za hivi karibuni, utawala wa Kizayuni umezidisha mashambulizi yake dhidi ya Wapalestina huku ukipuuza sheria za kimataifa na haki za binadamu.

Hujuma na mashambulizi hayo yamejibiwa na wapigania uhuru wa Kipalestina hususan katika mji wa Nablus.

Kuongezeka mapambano ya silaha ya makundi ya muqawama wa Palestina hususan katika miji miwili ya Nablus na Jenin ambayo ni ngome za muqawama katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kumewatia wasiwasi zaidi viongozi wa utawala ghasibu wa Israel.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *