Taasisi ya Haki za Binadamu ya Intisaf imeripoti kuwa watoto wa Kiyemeni zaidi ya milioni 12 wanahitaji misaada ya kibinadamu.
Saudi Arabia huku ikiungwa mkono na Marekani, Imarati na nchi nyingine kadhaa zilianzisha mashambulizi dhidi ya Yemen mwezi Machi 2015 na kuiwekea nchi hiyo mzingiro wa anga, baharini na nchi kavu. Uvamizi wa nchi hizo huko Yemen umepelekea maelfu ya Wayemeni kuuawa na kujeruhiwa makumi ya maelfu ya wengine huku mamilioni ya watu wakisalia wakimbizi.
Kwa mnasaba wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Watoto Wahanga wa Mizozo na Vita, Taasisi ya Kutetea Haki za Wanawake na Watoto ya Intisaf imetangaza kuwa: Watoto wa Yemen wanakabiliwa na matatizo mabaya zaidi ya kiakili, kimwili na kiafya, majeraha, mauaji na kuhama kuwa wakimbizi; kwa kadiri kwamba kutokana na uvamizi huo wa miaka minane dhidi ya Yemen, watoto milioni 12 na elfu 600 wa nchi hiyo wanahitaji misaada ya kibinadamu au uungwaji mkono.
Taarifa ya Taasisi ya Intisaf aidha imeeleza kuwa, Umoja wa Mataifa haujatekeleza majumuku yake ya kuwasaidia watoto huko Yemen kiasi kwamba tangu muungano wa Saudia na Marekani uivamie Yemen hadi sasa watoto 8,218 wameaga na au kujeruhiwa nchini humo.
Taarifa ya Taasisi ya Kutetea Haki za Wanawake na Watoto ya Intisaf imeongeza kuwa:Takwimu za karibuni zinaonyesha kuwa kiwango cha umaskini huko Yemen kimefikia asilimia 80; na watoto 8 kati ya kila watoto 10 wanaishi katika familia ambazo hazina mapato ya kutosha ya kujidhaminia mahitaji yao ya msingi na muhimu.