Makundi tofauti ya wananchi wa Palestina wamefanya ibada ya Swala ya Eid al-Fitr katika maeneo tofauti ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu Ijumaa asubuhi ya leo. Takriban watu 120,000 waliswali swala ya Idi katika Msikiti wa Al-Aqsa.
Licha ya utayarifu kamili wa jeshi la Kizayuni katika Jerusalem inayokaliwa kwa mabavu na kuunda vizuizi vya kijeshi na kutumwa vikosi vyenye nia ya ughasibu kwenye lango la Msikiti wa Al-Aqsa, usimamizi wa msikiti huu umetangaza kuwepo kwa wingi wa waumini katika msikiti huu.
Tovuti ya Arabi 21, ikinukuu uongozi wa Msikiti wa Al-Aqsa, ilitangaza kwamba askari wa Kizayuni waliokuwa kwenye lango la Msikiti wa Al-Aqsa, waliwakagua waumini na kuchukua vitambulisho vya baadhi yao.
Uongozi wa Msikiti wa Al-Aqsa pia ulifafanua kwamba milango ya msikiti huu iko wazi isipokuwa mlango wa al-Maghrabah – ambao Wazayuni wenye itikadi kali wanautumia kushambulia Msikiti wa Al-Aqsa.
Uongozi wa Msikiti wa Al-Aqsa ulikadiria idadi ya waumini katika Msikiti wa Al-Aqsa kuwa karibu watu 120,000 na ukabainisha kuwa Sheikh Omar Al-Kaswani, mkurugenzi wa Msikiti wa Al-Aqsa, ndiye msemaji wa sala ya Eid al-Fitr.
Sheikh Hefzi Abu Sunineh, Mkurugenzi wa Madhabahu ya Ibrahim, muda mfupi kabla ya swala hiyo alisema: “Madhabahu ya Ibrahim ni kitovu cha mji wa Hebroni, na matendo ya utawala unaoukalia kwa mabavu hayawezi kuleta mabadiliko yoyote katika moyo huu na mazingira yake. jeshi la utawala huu halitaruhusu Swala yoyote isiingie kwenye kaburi hili isipokuwa kupitia milango ya kielektroniki na ukaguzi.