Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amesema kuwa sera za uhasama za Washington ndiyo sababu ya kushuhudiwa mgogoro katika suala la kudhibiti silaha.
Maria Zakharova ameeleza kuwa: Wabunge wa Marekani wabunge wa Washington wanaendelea kujifanya kana kwamba, mgogoro wa udhibiti wa silaha hauhusiani na sera za uhasama za Washington mkabala wa Moscow. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia ameeleza haya akijibu matamshi ya Jake Sullivan Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani.
Zakharova ameongeza kusema kuwa: Tunafahamu kuwa hakuna nukta yoyote mpya ya msingi kuhusu udhibiti wa silaha inayoweza kuondoa wasiwasi wa Russia katika uwanja huo. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia aidha ameeleza kuwa: Hata kama Jack Sullivan amejaribu kuwasilisha mapendekezo ya Marekani katika vifurushi vya rangi zaidi ili kuishawishi Russia kufanya mazungumzo, lakini Washington inaendelea kupuuza sababu zilizopelekea kushuhudiwa hali ya mgogoro katika uwanja huo.
Maria Zakharova amesisitiza kuwa: Russia haijapinga njia za kisiasa na kidiplomasia za kudhamini usalamba ambazo zinaweza kutekelezwa kwa njia mbalimbali. Mwanadiplomasia huyo wa Russia ameongeza kuwa: Mbinu za udhibiti wa silaha unakua wenye taathira na kukubalika ikiwa pande zote zinataka ushirikiano sawa na wenye kujenga huku pande husika zikiteleza mikataba kwa uaminifu.
Itakumbukwa kuwa, Jake Sullivan Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Marekani alizitaka Moscow na Beijing kushiriki katika mazungumzo ya kudhibiti silaha licha ya kushuhudiwa mivutano kati ya Marekani na pande hizo.