Rais wa Ukraine alimtaka mwenzake wa Urusi wakae kwa ajili ya mazungumzo.
Katika ujumbe wa video uliotumwa kwenye chaneli yake ya Telegram, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelinsky alimwalika mwenzake wa Urusi, Vladimir Putin, kwa ajili ya kufanya mazungumzo.
Zelensky alinukuliwa na Sputnik ; “Ninataka kumwomba Rais wa Shirikisho la Urusi kwa mara nyingine tena tukae kwenye meza ya mazungumzo ili kuzuia vifo vya watu,”.
Ombi hilo linakuja siku moja baada ya Kiev kutangaza kuwa imekatisha uhusiano wa kidiplomasia na Moscow. “Ilirekodiwa katika historia asubuhi ya leo,” aliambia mkutano wa waandishi wa habari jana. Japo tarehe hii ni tofauti kabisa kwa nchi yetu na Urusi, na tulikatisha uhusiano wetu wa kidiplomasia na Urusi.
Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov amesisitiza kuwa Moscow iko tayari kujadiliana kuhusu Ukraine wakati wowote, punde tu jeshi la Ukraine litakapoweka chini silaha zake.”Tumeachwa peke yetu katika vita dhidi ya Urusi,” rais wa Ukrain alisema siku ya Ijumaa asubuhi, akizikosoa kwa uwazi nchi za Magharibi.
Aliandika katika ukurasa wake wa Twitter: ‘Ukraine imeachwa peke yake ikijitetea. Magharibi imebaki kuzungumza kuhusu msaada wake na inasema kwamba haijaondoka Kiev.